Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 21:04

Upinzani DRC waungana kumuondoa madarakani Rais Kabila


Kiongozi mkongwe wa upinzani nchini DRC, Etienne Tshisekedi
Kiongozi mkongwe wa upinzani nchini DRC, Etienne Tshisekedi

Vyama vya upinzani vinavyoongoza huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC vinasema vimejipanga chini ya mwamvuli mmoja unaoitwa “Ressembement” au “Rally” ili kumlazimisha Rais Joseph Kabila kuondoka madarakani.

Muhula wa pili wa Rais kabila unaisha mwishoni mwa mwaka huu. Ushirika mpya uliundwa wiki iliyopita huko Belgium na unajumuisha chama cha Union for Democracy and Social Progress-UDPS kinachoongozwa na kiongozi mkongwe wa upinzani, Etienne Tshisekedi, Dyanamic Opposition na G7 ambacho hivi karibuni kilimchagua gavana wa jimbo la Katanga, Moise Katumbi kama mgombea wake wa urais.

Vidiye Tshimanga ni Makamu Rais wa Alternative 2016 moja ya makundi yaliyotengeneza ushirika mpya. Alisema ushirika mpya utaongozwa na mwanasiasa mkongwe Etienne Tshisekedi.

XS
SM
MD
LG