Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Machi 26, 2025 Local time: 20:20

Upigaji kura waendelea Alhamisi DRC


Mpiga kura akishiriki kwenye zoezi hilo DRC.
Mpiga kura akishiriki kwenye zoezi hilo DRC.

Wapiga kura huko  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Alhamisi wanaendelea na upigaji kura kwenye uchaguzi mkuu uliogubikwa  na matatizo ya vifaa, na kupelekea  baadhi ya vituo vya kupigia kura kutokufunguliwa .

Taifa hilo masikini la Afrika ya Kati, na lenye utajiri mkubwa wa madini liliitisha uchaguzi wa rais, wabunge wa taifa na majimbo pamoja na madiwani. Rais Felix Tshisekedi mwenye umri wa miaka 60 anawania muhula wa pili madarakani, wakati kukiwa na changamoto za ukuaji wa uchumi na mfumuko mkubwa wa bei.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, upigaji kura wa Jumatano ulikumbwa na uchelewesho mkubwa kote nchini, wakati tume ya uchaguzi ikijaribu kusambaza vifaa vya kupigia kura kwenye baadhi ya vituo, muda mrefu baada ya zoezi hilo kuanza.

Baadhi ya vituo havikufunguliwa, na kuwafanya watu kushindwa kupiga kura zao. Kiongozi wa tume hiyo Denis Kaduma, kupitia televisheni ya kitaifa Jumatano usiku alisema kwamba wapiga kura kwenye maeneo ambayo wameshindwa kupiga kura hiyo jana watashiriki zote hilo Alhamisi.

Hata hivyo hakuna takwimu kamili iliyotolewa ya idadi ya vituo vilivyoathiriwa kote nchini.

Forum

XS
SM
MD
LG