Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 28, 2023 Local time: 06:27

Upigaji kura unaendelea katika jimbo la New Hampshire


Wakazi wakiingia na kutoka katika Ward 1, Manchester,jimbo la New Hampshire, Feb. 9, 2016.

Wakazi katika jimbo la New Hampshire ambako theluji inamwagika wanaendelea kupiga kura Jumanne katika uchaguzi wa awali wa kumteuwa mgombea atakayewakilisha chama chake katika kinyang’anyiro cha urais baadae mwaka huu.

Kabla ya upigaji kura huo uchunguzi wa kura za maoni katika jimbo la New Hampshire ulionesha Bernie sanders akishuka umaarufu lakini bado alikuwa anashikilia tarakimu mbili dhidi ya mpinzani wa ke Hillary Clinton wote wa chama cha democrat.

Upigaji kura ukiendelea huko nashua, New Hampshire, Feb. 9, 2016.
Upigaji kura ukiendelea huko nashua, New Hampshire, Feb. 9, 2016.

Bilionea Donald Trump anaonekana kuongoza dhidi ya wagombea wote wa chama cha republican kwa idadi kubwa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:44 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Yafuatayo ni mahojiano ya Mkamiti Kibayasi na Harrison Kamau akiwa New Hampshire kwenye zoezi hilo ambapo anaanza kuelezea hali ilivyo katika dakika za mwisho mwisho za upigaji kura kwenye uchaguzi wa awali jimboni humo.

XS
SM
MD
LG