Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:23

Upigaji kura kumchagua Waziri Mkuu Uingereza wacheleweshwa kudhibiti udukuzi


Waziri Mkuu Boris Johnson
Waziri Mkuu Boris Johnson

Hatua ya wanachama wa Conservtive nchini Uingereza kupiga kura kumtafuta Waziri Mkuu imechelewa baada ya idara ya ujasusi ya Uingereza kuonya kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kutokea udukuzi wakati wa upigaji kura.

Shirika la habari la the Telegraph limeripoti kwamba chama cha Conservative kimelazimika kubadilisha mpangilio wa uchaguzi huo.

Kura za wapiga kura 160,000 zinazosafirishwa kwa njia ya posta zinatarajiwa kuwafikia Agosti 11.

Aliyekuwa Waziri wa Fedha Rishi Sunak, na Waziri wa Mambo ya Nje Liz Truss wanapigiwa upatu mkubwa wa kumrithi Boris Johnson kama Waziri Mkuu wa Uingereza.

Ukusanyaji wa maoni unaonyesha kwamba Truss ana ufuasi mkubwa akilinganishwa na Sunak.

Mshindi atajulikana Septemba tarehe 5.

XS
SM
MD
LG