Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 13:55

Upigaji kura kudhibiti bunduki Marekani umegonga mwamba


Seneta Chris Murphy, wa Democrat kutoka jimbo la Connecticut. Washington, June 16, 2016.
Seneta Chris Murphy, wa Democrat kutoka jimbo la Connecticut. Washington, June 16, 2016.

Siku nane baada ya kutokea mauwaji mabaya ya bunduki katika historia ya Marekani yaliyosababisha vifo vingi kwa mara moja baraza la seneti limepiga kura kupinga mifululizo wa mapendekezo kadhaa ya kuweka vikwazo dhidi ya watu fulani wanaostahili kununua silaha na kupanua uchunguzi kwa wanunuaji kabla ya kununua bunduki.

Jumatatu jioni wa-Republican walizuia mapendekezo mawili ya muda mrefu ambayo wa-Democrat waliyarudisha tena kwa nguvu baada ya mfyatuaji risasi Omar Mateen aliyechochewa na itikadi za kundi la Islamic State kuuwa watu 49 waliokua ndani ya klabu ya mashoga wiki moja iliyopita katika mji wa Orlando kwenye jimbo la Florida.

Upigaji kura umefanyika siku kadhaa baada ya seneta wa Democrat, Chris Murphy wa jimbo la Connecticut kuchukua uongozi wa ukumbi wa seneta kwa saa 15 wiki iliyopita kutaka hatua zichukuliwe na wabunge dhidi ya ghasia za bunduki.

Ghasia za bunduki zinaongezeka nchini Marekani.
Ghasia za bunduki zinaongezeka nchini Marekani.

​"Magaidi hii leo wanatumia silaha kubwa za kushambulia badala ya mabomu ya kiyenyeji au ndege kuwashambulia wa-Marekani. Baada ya Septemba 11 tuliamua hatutaruhusu magaidi kutumia ndege kuwauwa raia. Basi hii leo wamehamia kwenye mashambulizi ya kutumia silaha. Watu wa Marekani hawatakata tamaa. Tutaangalia namna majadiliano haya yanavyokwenda kwa muda wa siku kadhaa zijazo lakini nitakueleza hivi, ni ushahidi tosha kwamba warepublicans wanajua kwamba wapo kwenye upande mbaya wa wapiga kura”.

Pendekezo moja lililokataliwa lingewazuia watu waliopo kwenye orodha ya serikali kuu wanaofuatiliwa kuhusiana na ugaidi ikiwemo wale wanaopigwa marufuku ya kusafiri na kununua bunduki. Pendekezo jingine litapanua uchunguzi wa lazima kwa wanunuaji wa silaha ikijumuisha maduka ya bunduki na uuzaji wa internet.

Nembo ya Republican.
Nembo ya Republican.

Wa-Republican walisema hawatapigia kura pendekezo lolote ambalo halikutoa maana kwa wale waliowekwa kwenye orodha ya ugaidi iliyofanyiwa uamuzi na serikali kuu.

Wakati huo huo mapendekezo mawili ya Republican yalipingwa siku ya Jumatatu. Moja litahitaji serikali kupata amri ya mahakama ili kuzuia washukiwa magaidi kuweza kupata bunduki na la pili ni kwamba litawaeleza kitengo cha sheria nchini Marekani wakati mtu anapofanyiwa uchunguzi kwa ugaidi katika miaka ya karibuni anaponunua bunduki.

Upigaji kura wa Jumatatu uliendeleza mlolongo wa wabunge kupinga hatua za kudhibiti bunduki hata baada ya kutokea matukio yaliyosababisha ufyatuaji risasi mbaya nchini humo.

XS
SM
MD
LG