Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 11:22

UNICEF yalaani ghasia na manyanyaso kwa watoto nchini Iran

UNICEF yalaani manyanyaso yaliyosababisha vifo kwa watoto nchini Iran
UNICEF yalaani manyanyaso yaliyosababisha vifo kwa watoto nchini Iran

Iran ni sehemu ya Mkataba wa Haki za Mtoto na shirika la kimataifa la utetezi wa watoto limesema katika taarifa yake kwamba viongozi nchini humo wana wajibu wa kuheshimu, kulinda na kutimiza haki za watoto kuishi, faragha, uhuru wa mawazo na kukusanyika kwa amani.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) lilitoa taarifa Jumapili likilaani "ghasia na manyanyaso ambayo yameripotiwa kusababisha vifo vya zaidi ya watoto 50 na kujeruhi wengine wengi wakati wa machafuko ya umma nchini Iran."

Shirika hilo limesema "lina wasiwasi mkubwa juu ya kuendelea kwa uvamizi na upekuzi unaofanywa katika baadhi ya shule" na kusema kuwa "shule lazima kila wakati ziwe sehemu salama kwa watoto".

UNICEF imeripoti kuwa "imewasilisha moja kwa moja wasiwasi wetu kwa mamlaka nchini Iran tangu visa vya kwanza vya majeruhi wa watoto kutokea kujibu maandamano hayo". Baadhi ya mashirika ya kutetea haki za binadamu yanaripoti kuwa takriban watoto 63 wameuawa katika maandamano hayo.

Iran ni sehemu ya Mkataba wa Haki za Mtoto na shirika la kimataifa la utetezi wa watoto limesema katika taarifa yake kwamba viongozi nchini humo wana wajibu wa kuheshimu, kulinda na kutimiza haki za watoto kuishi, faragha, uhuru wa mawazo na kukusanyika kwa amani.

UNICEF ambalo ni shirika lililoshinda Tuzo ya Amani ya Nobel limeitaka Iran "kuheshimu haki za watoto wote katika mkutano wa amani kama dhamana ya msingi bila kujali wao ni nani au wako wapi. Watoto na vijana wanapaswa kulindwa dhidi ya aina zote za madhara ambayo yanahatarisha sio tu maisha na uhuru wao lakini pia afya yao ya kiakili na kimwili".

XS
SM
MD
LG