Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 15:18

UNICEF inasema watoto milioni 4 bado wanahitaji misaada ya kibinadamu Pakistan


Mfano wa watoto wenye kuhitaji msaada nchini Pakistan
Mfano wa watoto wenye kuhitaji msaada nchini Pakistan

Onyo hilo kutoka kwa UNICEF linakuja wakati maafisa katika jimbo la mashariki mwa Pakistan la Punjab wanapambana na muda wa kuwahamisha watu kutoka maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko ya  mto Sutlej

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) limeonya kuwa mwaka mmoja tangu kutokea kwa mafuriko makubwa nchini Pakistan inakadiriwa watoto milioni 4 wanaendelea kuhitaji misaada ya kibinadamu na fursa ya huduma muhimu wakati uhaba wa fedha bado ni kikwazo katika hali ya kuponya.

Onyo hilo kutoka kwa UNICEF linakuja wakati maafisa katika jimbo la mashariki mwa Pakistan la Punjab wanapambana na muda wa kuwahamisha watu kutoka maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko ya mto Sutlej. Tangu Agosti Mosi waokoaji wamewahamisha zaidi ya watu 100,000 kutoka maeneo yaliyotelekezwa katika wilaya za Kasur na Bahawalpur.

Zaidi ya miezi sita iliyopita nchi kadhaa na taasisi za kimataifa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mjini Geneva ziliahidi zaidi ya dola bilioni 9 kuisaidia Pakistan kupata nafuu na kujijenga upya kutokana na mafuriko ya msimu wa joto uliopita.

Lakini ahadi nyingi zilikuwa katika mfumo wa mikopo kwa miradi ambayo bado iko katika hatua za maandalizi.

Forum

XS
SM
MD
LG