Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 11:53

UNHCR yasema wasomali milioni 7.5 watoroka makazi yao


watoto wa Somalia wakiwa wamejipanga mstari kusubiri msaada wa chakula
watoto wa Somalia wakiwa wamejipanga mstari kusubiri msaada wa chakula

Makadirio hayo ya UNHCR yamekuja huku makundi ya misaada yakiomba msaada mkubwa kwa ajili ya Somalia


Shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa mataifa, UNHCR limesema sasa ghasia na ukame vimetorosha wasomali milioni 7.5 katika makazi yao kwenda kwenye makambi ya ndani nchini humo au nje ya nchi.

Makadirio hayo ya UNHCR yamekuja huku makundi ya misaada yakiomba msaada mkubwa kwa ajili ya Somalia ambako ukosefu wa mvua umesababisha ukame mkubwa pamoja na vita vya wenyewe kwa wenye vya muda mrefu.

Shirika hilo limesema hivi sasa Somalia inakabiliwa vikali na kiwango kikubwa cha utapia mlo hasa kwa wakimbizi wengi. UNHCR imesema zaidi ya nusu nzima ya watoto wa Somalia wanawasili Ethiopia huku wakiwa na utapiamlo. Asilimia 40 wanakwenda Kenya.

Hata hivyo taarifa nyingine zinasema kwamba watoto hao wanaowasili katika nchi jirani wakiwa na afya duni wanafariki kwa muda wa masaa 24 licha ya kupatiwa huduma za dharura na malisho. Wakati huo huo shirika hilo la kuhudumia wakimbizi limeripoti kutokea mapigano baina ya wakazi na polisi karibu na kituo cha usambazaji wa chakula cha Daadab huko Kenya .

XS
SM
MD
LG