Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 02:54

UNHCR inasambaza misaada Sudan Kusini


Idara ya umoja wa mataifa ya kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) imesema inasambaza misadaa ya kuokoa maisha kwa zaidi ya familia 6,000.

Familia hizo ni zile ambazo zimekwama kutokana na mapigano katika jimbo la Yei River kwa kipindi cha miezi sita sasa.

Watu hao waliokoseshwa makazi ndani ya eneo hilo wamefurahia misaada lakini wanataka waruhusiwe kurudi kwa usalama katika nyumba zao ili waweze kuvuna mazao waliyopanda.

Mgao wa chakula wanao pokea sasa hauwatoshi.

Maafisa wa UNHCR wamesema zaidi ya familia 10,000 zilikoseshwa makazi katika kaunti ya Yei baada ya mapigano kutokea baina ya vikosi vya serekali na makundi ya upinzani yenye ushirika na makamu wa rais wa zamani Riek Machar.

XS
SM
MD
LG