Hatua hiyo ni muhimu katika kukabiliana na viwango vya juu vya njaa vinavyoendelea kushuhudiwa kote ulimwenguni. Mkuu wa program ya chakula kwa watoto wa shule kutoka WFP, Carmen Burbano, amesema kwamba serikali kote ulimwenguni zinaonekana kutambua umuhimu wa lishe bora kwa watoto kama suala linalohitajika kupewa kipaumbele licha ya janga linaloshuhudiwa kote ulimwenguni na hasa kwenye mataifa masikini.
Ripoti hiyo imeongeza kusema kwamba idadi ya watoto wanaofikiwa na chakula kupitia program hiyo imepita ile ya kabla ya janga la Covid-19. WFP imesema kwamba mwaka jana, watoto milioni 418 kote ulimwenguni walipokea chakula shuleni, likiwa ongezeko la watoto milioni 30 kulinganishwa na mwanzoni mwa 2020.