Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:46

UN yapeleka vikosi vya kulinda amani C.A.R


wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Jeshi la walinda amani la Umoja wa Mataifa Jumatatu litapelekwa huko Jamhuri ya Afrika ya kati , nchi ambayo imeharibiwa na ghasia za madhehebu na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa Zaidi ya miaka miwili.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeidhinisha jeshi linalojulikana kama MINUSCA kuchukua hatua zote muhimu kutekeleza mamlaka yake huko jamhuri ya afrika ya kati. Kwa wengi mjini Bangui hatua hii inamaanisha kuwa jeshi la umoja wa mataifa halitasita kutumia nguvu dhidi ya makundi yenye silaha.

Msemaji wa serikali ya jamhuri ya afrika ya kati Gaston Mackouzangba amesema kuwasili kwa jeshi hilo la umoja wa mataifa lenye vifaa itakuwa ni pigo kwa makundi yenye silaha.

Anasema ukiwa na watu elfu 12 wenye silaha na vifaa bora kuliko vile vya Jamhuri ya Afrika ya kati hiyo inatosha kushawishi waache vitendo vyao.

Mkuu wa chuo kikuu cha BANGUI Gustave bobossi –serengbe amesema maendeleo ya kiuchumi nchini humo yamedhoofika katika miaka ya hivi karibuni. Anasema mbali na kurejesha usalama na amani vikosi vya umoja wa mataifa vitakuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya ndani.

Amesema hakuna barabara wala hakuna mawasiliano , shule nyingi karibu ni kama vile hazipo. Kila kitu kiko katika kiwango cha sifuri , kwa hiyo kutakuwa na watu takriban watu elfu 10 wenye kila aina ya ujuzi.

Viongozi wengi wa makundi ya silaha pia wamesema wanakaribisha vikosi vya umoja wa mataifa.

Kwa mujibu wa umoja wa mataifa vikosi 7500 pekee ndio vitapelekwa Jumatatu kati ya vikosi elfu 12 vinavyotarajiwa . vikosi vingine elfu sita vya umoja wa afrika vilivyoko Jamhuri ya Afrika ya kati vitaungana na ujumbe wa umoja wa mataifa.

XS
SM
MD
LG