Baadhi ya mataifa hayo ni kama vile Bangladesh, China, India na Uholanzi yambayo yapo kwenye hatari ya kusombwa na kuhatarisha maisha ya takriban watu milioni 900 wanaoishi kwenye sehemu za nyanda za chini.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Guterres ametoa ripoti ya kutisha ikiwa ya kwanza ya aina yake mbele ya baraza la usalama la UN kuhusu tishio la amani na usalama wa kimataifa kutokana na kuongezeka kwa maji ya bahari , akionya kwamba hali hilo itaendelea kushuhudiwa licha ya viwango vya ongezeko la joto kudhibitiwa kwenye degree 1.5 Celcius kuendana na malengo ya kimataifa.
Kando na mataifa aliyosema yapo hatarini, Guterres pia ametaja miji mikuu kadhaa ambayo ipo hatarini kama vile Cairo, Lagos, Maputo, Bangkok, Dhaka, Jakarta, Mumbai, Shanghai. Copenhagen, London. Los Angeles, New York, Buenos Aires na Santiago.
Facebook Forum