Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 13:26

UN yapendekeza fidia kwa waathiriwa wa DRC


Mwanamke mmoja muathiriwa wa ubakaji huko DRC, akimfariji mtoto wake katika mji wa Fizi, February 20, 2011
Mwanamke mmoja muathiriwa wa ubakaji huko DRC, akimfariji mtoto wake katika mji wa Fizi, February 20, 2011

Jopo la ngazi ya juu linalotetea waathirika wa ubakaji limetoa wito kuwepo na mpango wa kuwapatia fidia maelfu ya wanawake wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC waliobakwa.

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema waathirika wa ubakaji wanakabiliwa na unyanyapaa, kukosa matibabu na ushauri nasaha, na hawapati msaada wa kutosha kuwashtaki wabakaji wao.

Ripoti hiyo ya kurasa 55 inaonesha kuwa waathirika wa ubakaji hutishiwa na wabakaji wao na kunyanyapaliwa na jamii. Jopo hilo lenye wanachama watatu walioteuliwa na tume ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa, lilisikiliza ushahidi kutoka kwa waathirika wa ubakaji wapatao 61 wakiwemo wanaume wane.

Jopo hili linapendekeza mfuko wa fedha uzinduliwe mara moja kuweza kuwasaidia waathiriwa wa ubakaji. Pia linapendekeza mfuko huo wa fedha uwe na wawakilishi kutoka DRC, Umoja wa Mataifa na wafadhili viongozi wa makundi ya kiraia na waathirika. Linasema waathirika ndio wanaojua mahitaji yao makuu na jinsi fedha hizo zinavyopaswa kutumiwa.

XS
SM
MD
LG