Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 19:20

UN kufunga vituo 4 vya kijeshi DRC


Walinda amani wa Umoja wa Mataifa
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa

Umoja wa Mataifa (UN) umetangaza kufunga vituo vyake vinne vya kulinda amani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatano katika eneo lenye vita huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Vituo hivyo ambavyo vitafungwa wiki ijayo viko katika maeneo ya Bukiringi, Geti, Mambasa na Bogoro, yote hayo yako katika jimbo la Ituri.

Bogoro ni eneo lililoshuhudia mauaji ya hali ya juu mwaka 2003 na kuacha takriban wanavijiji 200 wamuawa na kupelekea kesi ya jinai za kivita huko The Hague, na hatimaye kiongozi wa wanamgambo Germain Katanga aliyehukumiwa kifungo cha miaka 12.

“Tumelazimika kupunguza kwa kiwango kikubwa bajeti na wakati kazi inayotarajiwa kutekelezwa nasi ni kubwa katika katika eneo hilo. Ndiyo maana tumelazimika kupunguza idadi ya vituo vya kijeshi bila ya kuminya uwezo wa operesheni zetu,” amesema Julius Fondong, msemaji wa jeshi la UN linalojulikana kama Monusco.

Watu wengi katika eneo hilo la Bogoro wamepinga wazi kufungwa kwa vituo hivyo kwa sababu ya kuendelea kuwepo wasiwasi juu ya usalama wa eneo hilo.

XS
SM
MD
LG