Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:56

UN imetangaza hatua za kujaribu kuziba pengo dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa


Wanaharakati wa mabadiliko ya hali ya hewa
Wanaharakati wa mabadiliko ya hali ya hewa

Jukwaa jipya la WMO litaunganisha mifumo ya chaguo la nafasi na kuelezea sehemu zisizoeleweka juu ya wapi uzalishaji wa gesi chafu unaishia. Inapaswa kuleta matokeo ya haraka na kuelezea takwimu juu ya jinsi anga ya sayari inavyobadilika

Umoja wa Mataifa ulitangaza Jumatatu kwamba umechukua hatua muhimu kuelekea kujaribu kuziba pengo muhimu katika vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa, ufuatiliaji halisi wa gesi chafu. Shirika la Hali ya Hewa Duniani la Umoja wa Mataifa limekuja na miundombinu mipya ya ufuatiliaji wa gesi chafu duniani ambayo inalenga kutoa njia bora za kupima uchafuzi wa joto duniani na kusaidia kufanya maamuzi ya msingi ya sera.

Jukwaa jipya la WMO litaunganisha mifumo ya chaguo la nafasi na kuelezea sehemu zisizoeleweka juu ya wapi uzalishaji wa gesi chafu unaishia. Inapaswa kuleta matokeo ya haraka na kuelezea takwimu juu ya jinsi anga ya sayari inavyobadilika. "Tunajua kutokana na vipimo vyetu kwamba viwango vya gesi chafu katika anga viko juu," mkuu wa WMO, Petteri Taalas alisema. Gesi kuu tatu chafu ni Carbon Dioxide, methane na Nitrous Oxide. kati ya hizo Carbon Dioxide (CO2) inachangia kiasi cha asilimia 66 ya madhara ya joto-joto katika hali ya hewa.

"Ongezeko la viwango vya Carbon Dioxide (CO2) kutoka 2020 hadi 2021 lilikuwa kubwa kuliko kiwango cha wastani cha ukuaji katika muongo mmoja uliopita, na methane ilishuhudiwa kupanda kwa kiwango kikubwa zaidi mwaka hadi mwaka tangu vipimo vilipoanza," Taalas alisema.

Mkataba wa Paris wa mwaka 2015 juu ya mabadiliko ya hali ya hewa ulishuhudia nchi zikikubaliana kudhibiti ongezeko la joto duniani ikiwa chini ya nyuzi mbili za Celsius ambapo ni juu ya viwango vilivyopimwa kati ya 1850 na 1900 na 1.5C ikiwa inawezekana.

XS
SM
MD
LG