Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 00:59

Umoja mataifa yahimiza amani Burundi


Mwanajeshi akifanya ulinzi mjini Bujumbura, Burundi.
Mwanajeshi akifanya ulinzi mjini Bujumbura, Burundi.

Kutokana na matukio ya hivi karibuni, taifa hilo linaonekana kuchukuwa mwelekeo mpya na kuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, na mivutano sasa inajitokeza mjini Bujumbura.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:35 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kamishna wa haki za binadam wa umoja mataifa ameisihi serikali ya Burundi na wapinzani kurudi nyuma kabla mzozo uliopo sasa kugeuka na kuwa vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe.

Afisa huyo wa haki za binadam wa umoja mataifa Zeid Ra’ad al Hussein anasema anashutushwa na maendeleo ya karibuni yanayojitokeza katika mzozo wa Burundi. Afisa huyo wa umoja mataifa anazungumzia matukio ya umwagaji damu siku ya ijumaa pale watu wenye silaha waliposhamulia kambi tatu za kijeshi katika mji mkuu, na kuchochea mapigano makali ambapo watu takriban watu 87 waliuawa.

Msemaji wa kamishna huyo Cecile Pouilly anasema vikosi vya usalama vilfanya msako wa majumbani na kuwakamata mamia ya vijana. Kuna ripoti kuwa vikosi vya usalama huwenda waliwauwa baadhi ya wale waliokamatwa.

Bi Pouilliy anasema, kutokana na matukio ya hivi karibuni, taifa hilo linaonekana kuchukuwa mwelekeo mpya na kuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, na mivutano sasa inajitokeza mjini Bujumbura.

Baada ya miaka kadhaa ya Amani, Burundi imechukuwa mwelekeo wa kuwa na mauaji mwezi April, pale rais Pierre Nkuruzinza alipotangaza mipango yake ya kuwania muhula wa tatu , jambo ambao wakosoaji wanaliona ni kinyume cha katiba. Maandamno ya ghasia yalizuka na kuondoka, hivi karibuni yanaonekana kuongezeka.

Idara ya kuhudumia wakimbizi ya umoja mataifa inaeleza kuwa Zaidi ya warundi elfu mia 220 wamechukuwa hifadhi katika nchi jirani mwaka huu.

Pouilly ameambia sauti ya America kuwa usalama mjini Bujumbura ni mbaya sana na wafuatiliaji wa umoja mataifa hawajaweza kupata takwimu halisi za kile kilichotokea ijumaa.

Bi Pouilliy anasema serikali inaeleza kuwa idadi ya washambuliaji ambao walihusika katika ghasia za ijumaa ilikuwa takriban watu 150 na kwamba 79 kati yao waliuwawa. Lakini baadhi ya watu wanasema kuwa idadi ya majeruhi wa kiraia huwenda ikawa Zaidi ya mia 2. Lakina anasema, hatuna njia ya kuthibitisha tuhuma hizi za idadi.

Kamishna Zeid anazisihi pande zote kufanya kila wawezalo kusitisha ghaisa. Anatowa wito kwa serikali na upinzani kujihusisha katika majadiliano.

Leo baraza la haki za binadam la umoja mataifa litafanya kikao maalum juu ya Burundi katika juhudi za kufafanua matukio na kuzia hali kusambaa zaidi.

XS
SM
MD
LG