Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 22:16

UN, AU, EU wakutana kutafuta suluhisho la Burundi


Wananchi wakipigana wenyewe kwa wenyewe kutokana na itikadi za vyama vyao.
Wananchi wakipigana wenyewe kwa wenyewe kutokana na itikadi za vyama vyao.

Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Umoja wa ulaya wanatoa wito wa mazungumzo kati ya serikali ya Burundi na upinzani ili kuweza kutatua matatizo ya kisiasa nchini humo.

Katika taarifa ya pamoja Alhamis, maafisa wa vyeo vya juu kutoka taasisi zote tatu walisema ni vyema pande hizo zikutane haraka, ama kwenye mji mkuu wa Ethiopia au Uganda chini ya mpatanishi wake Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kwa pamoja kupitisha azimio Alhamis la kutoa wito wa kumalizika ghasia nchini Burundi na kitisho cha vikwazo dhidi ya mtu yeyote ambaye anakuwa kizuizi cha kupatikana amani nchini humo.

Waandamanaji wakipinga muhula wa tatu madarakani wa Rais Nkurunziza
Waandamanaji wakipinga muhula wa tatu madarakani wa Rais Nkurunziza

Hatua hiyo inaelezea wasi wasi kuhusu kuongezeka kwa ukosefu wa usalama nchini Burundi na ukosefu wa mashauriano miongoni mwa vyama hivyo.

Wanadiplomasia mjini New York nchini Marekani walisema Umoja wa Mataifa wataweza kuharakisha kupeleka walinda amani nchini Burundi kama hali ya utulivu haitarejea haraka katika taifa hilo lililopo Afrika Mashariki.

Maafisa nchini Burundi hata hivyo wanasema nchi haipo kwenye hali mbaya kihivyo na kwamba hakuna nafasi ya kutokea mauaji ya umma.

“Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana pamoja wiki hii ili kuhakikisha kwamba tunafanya kila liwezekanalo kuongeza shinikiza kwa maafisa mjini Bujumbura na kuonya dhidi ya hatari ya mauaji ya umma”, alisema Jumatano balozi wa Uingereza, Mathew Rycroft.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza akiwa mjini Bujumbura, May 17, 2015.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza akiwa mjini Bujumbura, May 17, 2015.

Umoja wa Afrika pia utaweza kuingilia mzozo wa Burundi kwa kupeleka kikosi cha kulinda amani.

Ghasia zilizuka mwezi April wakati Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza alipotangaza kwamba atawania muhula wa tatu madarakani, hatua ambayo upinzani iliiita ni kinyume cha katiba. Bwana Nkurunziza alichaguliwa tena kuongoza nchi hiyo mwezi Julai katika upigaji kura ambao upinzani uliususia.

XS
SM
MD
LG