Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 20:41

Nigeria yataja mshukiwa wa kupanga mabomu UN


Shambulizi la bomu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Abuja, Nigeria
Shambulizi la bomu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Abuja, Nigeria

Maafisa wa usalama nchini Nigeria wamemtaja mshukiwa aliyesaidia kupanga shambulizi la mabomu katika makao makuu ya UN mjini Abuja

Maafisa wa usalama nchini Nigeria wanasema mtu mmoja mwenye uhusiano na kundi la al-Qaida alisaidia kupanga shambulizi la mabomu lililotokea wiki iliyopita kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Abuja ambapo watu 23 waliuwawa.

Idara ya ulinzi nchini Nigeria ilisema Jumatano kwamba Mamman Nur, mwanachama wa kundi la ki-Islam lenye msimamo mkali la Boko Haram, alipanga shambulizi huku akishirikiana na washukiwa wawili wengine ambao wamekamatwa.

Taarifa inasema Nur, hivi karibuni alirudi kutoka Somalia ambapo wakala wa al-Qaida wanalisaidia kundi la uasi la al-Shabab kupambana na serikali ya Somalia.

Nur bado hajulikani alipo. Maafisa nchini Nigeria hawakuwaelezea washukiwa wawili waliopo kizuizini lakini walisema ni wanachama wa kundi la Boko haram na wametoa taarifa ya uthibitisho.

Ijumaa iliyopita, muuaji mmoja wa kujitolea alilipua bomu moja ndani ya gari kwenye eneo la Umoja wa Mataifa mjini Abuja, na kuwajeruhi zaidi ya watu 80 na kusababisha vifo vya watu 23.

Mtu mmoja ambaye alijitambulisha mwenyewe kama msemaji wa kundi la Boko Haram aliiambia Sauti ya Amerika kwamba kundi hilo lilihusika kwa shambulizi.

Kundi la Boko Haram ambalo jina lake linamaanisha ‘elimu ya magharibi ni haram’, limekuwa likilalamikiwa kufanya mifululizo ya mashambulizi ya mabomu na kuwafyatulia risasi maafisa wa vyeo vya juu huko kaskazini masharini ya Nigeria, hasa katika jimbo la Borno. Kundi hilo pia limedai kuhusika kwa mashambulizi mjini Abuja, likiwemo shambulizi la bomu la mwezi June nje ya makao makuu ya polisi nchini Nigeria.

Kundi hilo linataka mfumo wa sheria ya ki-Islam utumiwe zaidi nchini Nigeria. Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameapa kuongeza usalama na kudhibiti ugaidi nchini humo.


XS
SM
MD
LG