Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 10:02

Umoja wa vyama vya wafanyakazi wa bandari India unaitisha mgomo


Mojawapo ya shughuli zinazofanywa katika bandari za India.
Mojawapo ya shughuli zinazofanywa katika bandari za India.

Mgomo wa wafanyakazi wa bandari nchini India unaweza kuzidisha msongamano uliopo katika bandari za Asia na Ulaya.

Kundi la umoja wa vyama vya wafanyakazi wa bandari nchini India limeitisha mgomo kuanzia Agosti 28 wakitaka kutatuliwa mara moja kwa marekebisho ya mishahara na mafao ya pensheni, kulingana na barua iliyotiwa saini na wanachama wake.

Mgomo wa wafanyakazi wa bandari nchini India unaweza kuzidisha msongamano uliopo katika bandari za Asia na Ulaya, na kusababisha uchelewesho wa usafirishaji, na unaweza kuwa na athari ya kimataifa kwa biashara na uchumi.

Wizara ya usafirishaji ya nchi hiyo iliunda kamati ya pande mbili kuhusu ya mashauriano ya mishahara inayoangazia pande mbili hapo Machi 2021, na wafanyakazi waliwasilisha madai yao miezi sita baadaye, kabla ya kumalizika kwa makubaliano ya awali Desemba mwaka huo-huo, kulingana na barua hiyo.

Ingawa kamati ya majadiliano ya mishahara ilikutana mara saba, ilishindwa kutimiza matakwa ya wafanyakazi wa bandari, barua hiyo ilisema. Kundi hilo la wafanyakazi lilikubali kuitisha mgomo baada ya mkutano wa mwezi huu huko Thoothukudi, mji wa bandari uliopo kusini mwa jimbo la Tamil Nadu.

Forum

XS
SM
MD
LG