Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 21:09

Umoja wa Ulaya utasitisha sehemu ya mafunzo yake kwa wanajeshi Mali


Wanajeshi wa Mali wakipiga doria na wanajeshi wa Ufaransa katika mji wa Menaka, Mali
Wanajeshi wa Mali wakipiga doria na wanajeshi wa Ufaransa katika mji wa Menaka, Mali

Umoja wa Ulaya utasitisha sehemu ya mafunzo yake kwa wanajeshi wa Mali, mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell alisema Jumatatu, akielezea  ukosefu wa dhamana kutoka kwa mamlaka ya Mali kwamba wakandarasi wa kijeshi wa Russia hawataingilia kazi hiyo.

Uamuzi huo huenda ukaongeza wasiwasi wa kimataifa kuhusu muda wa kuendelea kuwepo kwa tume ya kulinda amani wa Umoja wa Mataifa (MINUSMA) na Umoja wa Ulaya EUTM na EUCAP, baada ya Ufaransa na washirika wake kuanza kujiondoa Mali mapema mwaka huu.

“Tumeamua kusimamisha kwa muda, kusitisha, baadhi ya miundo ya shughuli zeyu za mafunzo nchini Mali zinazolenga vitengo vya kijeshi vya walinzi wa kitaifa wa Mali," Borrell aliuambia mkutano wa waandishi wa habari kufuatia mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa EU.

"Hakuna uhakikisho wa kutosha wa usalama kutoka kwa mamlaka ya Mali juu ya kutoingilia kati kwa kundi maarufu la Wagner," Borrell alisema, ingawa aliongeza Umoja wa Ulaya haujitoi nchini humo.

XS
SM
MD
LG