Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 02:57

Umoja wa Ulaya umekataa pendekezo la Misri la kupunguza uzalishaji wa gesi chafu


Mkutano unaojadili hali ya hewa (COP27) huko Sharm El-Sheikh nchini Misri
Mkutano unaojadili hali ya hewa (COP27) huko Sharm El-Sheikh nchini Misri

Mazungumzo hayo yamekwama kufuatia wito kwamba mataifa tajiri wachafuzi wa hewa wanatoa ufadhili wa "hasara na uharibifu" kwa nchi zilizokumbwa na majanga ya hali ya hewa na pia juu ya matarajio ya kukabiliana na ongezeko la joto duniani

Mazungumzo ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa hayakwenda vizuri Jumamosi wakati Umoja wa Ulaya ulipokataa pendekezo la nchi mwenyeji Misri kwa ukosefu wa matarajio ya kupunguzwa uzalishaji wa gesi chafu na kuonya kuwa ni afadhali kuondoka bila makubaliano yoyote kuliko kuwa na makubaliano mabaya.

Takriban wawakilishi 200 wa nchi wamekusanyika katika mkutano wa COP27 nchini Misri kwa wiki mbili kwa lengo la kusukuma mbele hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa wakati dunia ikikabiliwa na hali mbaya sana ya hewa.

Lakini mazungumzo hayo yamekwama kufuatia wito kwamba mataifa tajiri wachafuzi wa hewa wanatoa ufadhili wa "hasara na uharibifu" kwa nchi zilizokumbwa na majanga ya hali ya hewa, na pia juu ya matarajio ya kukabiliana na ongezeko la joto duniani.

Baada ya mashauriano kurefushwa usiku kucha kufuatia siku rasmi ya mwisho iliyokuwa Ijumaa, Umoja wa Ulaya ulikataa rasimu ya waraka kutoka Misri.

Makamu wa Rais wa kamisheni ya Ulaya, Frans Timmermans amesema Umoja wa Ulaya "ni bora ukose matokeo mbadala kuliko kuwa na matokeo mabaya" na ulikuwa tayari kuondoka kwenye mazungumzo kabisa.

Lakini ameongeza kuwa umoja huo wenye mataifa wanachama 27 bado una matumaini ya kupata matokeo mazuri.

Umoja wa Ulaya unataka COP27 kuwa na matamshi makali juu ya kupunguza uzalishaji wa gesi chafu na kuthibitisha lengo la matarajio ya kupunguza ongezeko la joto duniani hadi nyuzi joto 1.5 kutoka viwango vya kabla ya viwanda.

XS
SM
MD
LG