Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:40

Umoja wa ulaya kuanzisha operesheni za Mediterranean


Wafanyakazi wa kitengo cha majini cha Italy kwenye boti ndogo wakiokoa wahamiaji kwenye bahari ya Mediterranean, May 3, 2015.
Wafanyakazi wa kitengo cha majini cha Italy kwenye boti ndogo wakiokoa wahamiaji kwenye bahari ya Mediterranean, May 3, 2015.

Umoja wa Ulaya ulitangaza Jumatatu kuwa imezindua operesheni za majini zinazolenga wasafirishaji biashara haramu ya watu na wafanya biashara magendo wanaobeba watu kuvuka bahari ya Mediterranean kuelekea ulaya.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini aliwaambia waandishi wa habari mjini Luxembourg kwamba operesheni hiyo kwanza itajumuisha taarifa zilizokusanywa pamoja na kufanya doria kwenye maji ya kimataifa ili kujaribu kunasa na kuangalia mitandao ya wafanya magendo. Alielezea kwamba lengo ni kutokomeza kazi za wafanya biashara ya magendo ambao wanawachukua wahamiaji kwenye safari za hatari ambazo zimesababisha watu 2,000 kufariki mwaka huu.

Federica Mogherini
Federica Mogherini

"Wacha niwe muwazi, walengwa sio wahamiaji. Walengwa ni wale watu ambao wanatengeneza fedha kwa maisha yao na mara kwa mara kwenye vifo vyao”, Mogherini alisema. “Ni sehemu ya juhudi zetu za kuokoa maisha”.

Maafisa wa Ulaya wamekuwa wakifanya kazi kupata suluhisho juu ya namna ya kukabiliana na mmiminiko wa zaidi ya wahamiaji 100,000 mwaka huu wengi wao wakiwa wamewasili nchini Ugiriki na Italy baada ya kukimbia vita, umaskini na manyanyaso ya kisiasa nchini mwao.

Hatua nyingine iliyopendekezwa ya operesheni ya Umoja wa Ulaya itakuwa kupanua operesheni hizo kuingia eneo la Libya ambalo ni moja ya vituo vikuu vya kuanzia safari. Lakini hilo litahitaji idhini kutoka kwa maafisa wa Libya na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

XS
SM
MD
LG