Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 19:33

Umoja wa Mataifa waalani mashambulizi ya al-Shabab


Wapiganaji wa Al-Shabab .
Wapiganaji wa Al-Shabab .

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameshutumu wanamgambo wa al- Shabab

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameshutumu wanamgambo wa al- Shabab nchini Somalia kwa kuvamia afisi za baadhi ya makundi ya kutoa misaada ya kibinadamu Jumatatu na kupiga marufuku shughuli zao nchini humo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alishtumu vikali uporaji wa mali na vifaa vya makundi ya kutoa misaada uliofanywa na kundi hilo la al-Shabab, huku naibu katibu mkuu wa maswala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa Valerie Amos akionya kuwa huenda baa la njaa likarejea katika baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na ukame nchini humo ikiwa shughuli za kutoa misaada zitavurugwa. Maafisa hao wawili pia walishtumu marufuku iliyotangazwa na wanamgambo hao wa al-Shabab dhidi ya taasisi 16 za kimataifa zinazotoa misaada katika maeneo wanayodhibiti. Msemaji wa al-Shabab alishtumu makundi hayo akisema kuwa yameonyesha kuegemea upande mmoja kisiasa na kwamba shughuli zao si halali nchini humo. Lakini mashirika kama vile Kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu na lile la madakatari wasio na mipaka wataruhusiwa kuendelea na shughuli zao.

XS
SM
MD
LG