Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:20

Umoja wa Mataifa unatoa wito wa kuhakikisha usalama kwa waandishi habari


Bango la UNESCO kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari 2013.
Bango la UNESCO kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari 2013.
Umoja wa mataifa ulitowa wito wa kuchukuliwa hatua ili kuhakikisha usalama wa waandishi wa habari katika kila nchi, siku ya Ijuma katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habrai Dunia. Wito huo ulitolewa na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki-Moon aliyetangaza kuwa “inapokuwa salama kuzungumza, dunia nzima inafaidika”.

“Kila siku uhuru wa kuzungumza unakabiliwa na vitisho vipya. Kwa sababu wanasaidia kuhakikisha uwazi na uwajibikaji katika masuala ya umma, waandishi wa habari mara kwa mara wanakuwa shabaha ya kushambuliwa”, alisema katibu mkuu Ban na Irina Bakova mkurugenzi mkuu wa idara ya Umoja wa mataifa kwaajili ya masuala ya elimu, sayansi na utamaduni-UNESCO katika ujumbe wa pamoja kusheherekea Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani inayoadhimishwa kila mwaka Mei 3.

“Wafanyakazi wengi wa vyombo vya habari wanataabika kutokana na kunyanyaswa, vitisho na ghasia. Wengi wanakabiliwa na hali ya kukamatwa kiholela na kuteswa, mara nyingi bila ya kupata msaada wa kisheria. Lazima tusimame imara kukabiliana na ukosefu wa usalama na ukosefu wa haki za sheria”, walisema Ban na Bakova.

UNESCO na washirika wote wa mashirika yote huru ya vyombo vya habari wanatoa wito wa kuwepo ulinzi bora kwa waandishi wa habari duniani kote. Inasema waandishi wa habari 121 waliuwawa duniani kote mwaka 2012 takribani mara mbili ya idadi kulingana na mwaka 2010 na mwaka 2011.
please wait

No media source currently available

0:00 0:19:45 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

UNESCO na washirika wake wanalenga kuhakikisha usalama na kupambana na tabia ya kutohukumiwa uhalifu unaotendwa dhidi ya waandishi wa habari. Mwezi Machi mwaka huu watu wenye silaha jijini Dar es Salaam nchini Tanzania walimshambulia na kumpiga mhariri wa gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda hadi kuzimia. Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika inaripoti kuwa mhariri huyo alipoteza jino, kucha na jicho moja.

Absalom Kibanda mwandishi habari wa Tanzania Daima
Absalom Kibanda mwandishi habari wa Tanzania Daima
Kamati ya kuwalinda waandishi wa habari-CPJ inasema mauaji ya waandishi wa habari 80 bado hayajatatuliwa tangu mwaka 1992. Wakati huo huo waandishi wa habari 41 barani Afrika wataadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani wakiwa gerezani.

CPJ inasema nchi tano zinazoongoza zenye idadi kubwa ya kesi zisizotatuliwa au kinga kwa washambuliaji zilikuwa Iraq, Somalia, Philippines, Sri lanka na Colombia. Nigeria ilikuwa namba 11.

UNESCO na makundi ya kutetea haki za waandishi wa habari yanalengo la kuongeza viwango vya kulinda uhuru wa vyombo vya habari na hatua za mpango wa Umoja wa mataifa juu ya usalama wa waandishi wa habari na suala la kinga.

Mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa ulibuni mei 3 kama siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani mwaka 1993. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “usalama wa kuzungumza: kuimarisha uhuru wa kujieleza katika vyombo vyote vya habari” inalengo la kuhamasisha hatua ya kimataifa kulinda usalama kwa waandishi wa habari wote duniani na kuvunja mzunguko wa kutohukumiwa vitendo vya uhalifu dhidi yao.
XS
SM
MD
LG