Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 03:17

UN yakubali kulaumiwa mauaji ya Sudan Kusini


Msemaji wa Idara ya Amani ya Umoja wa Mataifa amesema kuwa Umoja huo umekubali kulaumiwa kwa kutochukua hatua za dharura wakati wa mauwaji ya mwezi Februari ya watu waliokoseshwa makazi mwezi kwenye mji wa Malakal ulioko Sudan Kusini.

Nick Birnback amesema kuwa baadhi ya walinda amani hawakuchukua hatua kwa wakati kulinda watu hao walioshambuliwa na watu wenye bunduki Februari 17 na 18 wakiwa kwenye eneo la ulinzi wa raiya.

Wakati huo, Umoja wa Mataifa ulikuwa na vikosi vya wanajeshi kutoka Rwanda, Ethiopia na India mjini Malakal.

Watu 30 waliuwawa wakati wa shambulizi hilo huku wengine 123 wakijeruhiwa. Kwa sasa Umoja wa Mataifa unajadiliana tukio hilo na mataifa yaliotoa vikosi vya UNMISS kuhusu mafunzo na kuhusika kwao wakati wa shambulizi hilo.

XS
SM
MD
LG