Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 19, 2025 Local time: 17:49

Umati wa watu wenye hasira wavamia kituo cha polisi Pakistan na kumuua mfungwa


Maafisa wa polisi wa Pakistan wakimpiga muandamanaji wakati wa vurugu huko Islamabad, Pakistan.Sept, 21, 2012.
Maafisa wa polisi wa Pakistan wakimpiga muandamanaji wakati wa vurugu huko Islamabad, Pakistan.Sept, 21, 2012.

Umati wa watu wenye hasira katikati mwa Pakistan ulivamia kituo cha polisi Jumamosi na kumkamata mfungwa anayekabiliwa na mashtaka ya kukufuru na kumnyonga .

Tukio hilo lilitokea huko Nankana Sahib, mji wa mbali katika jimbo la Punjab lenye idadi kubwa ya watu katika nchi hiyo yenye Waislamu wengi.

Maafisa wa polisi walisema muathirika huyo aliyetambulika kwa jina la Muhammad Waris ametiwa mbaroni kwa madai ya kuidharau Quran. Walisema habari za madai ya uhalifu huo ziliwakasirisha wakazi na mamia ya wakazi hao baadaye walizunguka kituo cha polisi, wakitaka mshukiwa huyo akabidhiwe kwao.

Kwa kuzidiwa na umati mkubwa, maafisa wa polisi walikimbia kituo hicho. Waandamanaji walimkamata mtu huyo na kumburuta hadi barabarani ambako walimpiga hadi kufariki dunia. Msemaji wa polisi baadaye aliwaambia wanahabari kwamba vikosi vya polisi viliweza kuuzuia umati huo na kuuchoma moto mwili huo.

Video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha waandamanaji wakiuburuta mwili wa mwathirika huyo uchi mitaani

Taarifa ya polisi wa jimbo hilo ilisema kuwa watumishi waandamizi katika kituo cha polisi wamesimamishwa kazi kwa kushindwa kuzuia shambulio hilo na uchunguzi wa haraka wa tukio hilo umeamriwa.

XS
SM
MD
LG