Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 19:26

Umaarufu wa Trump washuka kabla ya kuingia madarakani


Rais mteule Donald Trump
Rais mteule Donald Trump

Gazeti la Washington Post-ABC News Poll limesema Jumanne, siku tatu kabla ya Trump kuapishwa Ijumaa, kwamba ni rais aliyepoteza umaarufu vibaya sana ukilinganisha na marais angalau saba waliokuwa wamechaguliwa miaka saba nyuma.

Maoni yaliokusanywa na Shirika la CNN na gazeti la Post-ABC yanaonyesha Trump anakubalika kwa asilimia 40, ikiwa ni nusu ya takwimu za Rais Barack Obama wakati anachukua madaraka na pia chini ya asilimia 61 inavyoonyesha wakati sasa anaachia madaraka.

Maoni hayo yanaonyesha akiwa ni kiongozi mwenye umaarufu wa chini kabisa kuliko kiongozi yeyote aliyetangulia kwa miaka mingi jambo ambalo yeye mwenyewe amelikanusha.

Utafiti wa gazeti hilo na ule uliofanywa na CNN katika siku za karibuni umeonyesha kuwa wapiga kura wa Marekani wamekuwa na maoni hasi juu ya Trump katika mpito wa kubadilishana madaraka mara tu baada ya uchaguzi wa Novemba, kitu ambacho kimeonyesha kuporomoka kwa umaarufu wake kuliko rais wengine.

Lakini Trump amesema katika ujumbe wake wa Twitter: “Watu hawa hawa waliotengeneza uongo wakati wa uchaguzi, na wakawa wamekosea sana, ndio ambao wanatumika kutoa maoni kuhusu umaarufu wangu.” Aliongeza kuwa hawa wamechakachua maoni kama ilivyokuwa katika uchaguzi.

Rais mteule amesema, “ Watu wanamiminika Washington kwa idadi kubwa. Wapanda pikipiki wa Trump wako njiani. Itakuwa siku kubwa Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi!”

XS
SM
MD
LG