Kupitia taarifa iliyotolewa, WHO imesema kwamba kuwepo na changamoto za afya ya akili hakuwezi kuchukuliwa kama sababu ya kumnyima mtu haki yake ya kibinadamu, au kumuengua kwenye maamuzi muhimu kuhusiana na afya yake. Licha ya hilo, watu wenye matatizo ya kiakili kote ulimwenguni wameendelea kushuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, taarifa imeongeza.
WHO imesema kwamba mtu mmoja kati ya kila 8 ulimwenguni anaishi na tatizo la afya ya akili, ambayo huenda ikaathiri afya ya mwili, hali yao ilivyo, pamoja na kuathiri maisha yao kwa ujumla. Siku ya kimataifa ya afya ya akili ilianzishwa 1992 na shirikisho la kimataifa la Afya ya Akili, na tangu wakati huo imeendelea kupata umaarufu, wakati watu zaidi wakiendelea kuhamasika kuhusu umuhimu wa afya ya akili katika uzima wa mwili wa binadamu.
Shirika hilo limekuwa likihamasisha kuhusu mahitaji ya watu wanaopitia changamoto za afya ya akili tangu 1948.
Forum