Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 05:59

Ukuaji wa mitandao ya kijamii imesababisha wasiwasi katika vyombo vya habari Afrika


Waandishi wa habari na wageni wakiwa kwenye studio za Radio na televisheni ya Lisanga (RLTV), Kinshasa, DRC. June 21, 2018
Waandishi wa habari na wageni wakiwa kwenye studio za Radio na televisheni ya Lisanga (RLTV), Kinshasa, DRC. June 21, 2018

Wamiliki na wakurugenzi wa vyombo vya habari barani afrika wameonyesha wasiwasi wa hatari inayosababishwa na mifumo ya kidigitali kwenye sekta ya habari.

Kutokana na teknolojia ya habari na mifumo ya kidigitali, sekta ya habari inakabiliwa na habari potofu na changamoto nyingine.

Kutokana na mapinduzi yanayoshuhudia kwenye ulimwenguni wa kidigitali wamiliki wa vyombo vya habari wanaonekana kukuna vichwa kuhusu ni nini la kufanya ili viendelee kutosheleza mahitaji ya wasikilizaji wa Radio na watazamaji wa televisheni kwenye nchi mbalimbali.

Hii inatokana na ukweli kwamba wasikilizaji na watazamaji wengi wanaendelea kuhamia kwenye mitandao ya kijamii, kundi kubwa la wasikilizaji likiwa ni vijana ambao kimsingi ndiyo sehemu kubwa ya jamii.

Mikakati ya kushindana na mitandao ya kijamii

Sasa wakurugenzi wa mashirika ya umma barani Africa na wadau kwenye huduma ya kutoa intaneti wanajadiliana mikakati ya kuchukua ili kushindana na mitandao ya kijamii, inayotishia kuondoa katika biashara vyombo vya habari vya kawaida.

Mitando ya kimaii kama facebook, you tube, inatumika kupeperusha habari moja kwa moja. Wakati mwingine, mitandao hiyo inaonyesha habari pindi zinapotokea bila kuhaririwa na hivyo kupata watazamaji wengi kuliko vyombo vya habari vya kawaida.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la utangazaji nchini Rwanda ambaye pia ni mwenyekiti wa shirikisho la vyomvo vya umma barani afrika Arthur, anasema

“Vyombo vya habari vipo lakini ukiangalia takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kwamba wastani wa dunia wa kutazama televisheni umeshuka kwa kiwango cha asilimia 3%. Ngoja niwaulize hata sisi tuliomo humu ni watu wangapi ambao wanapata muda wa kukaa mbele ya runinga na kutazama…ona sasa ni wachache mno…nadhani mstakabari wa Radio na Televisheni una matatizo.”

Je, Radio na televisheni vinapoteza umaarufu?

Hata hivyo mjadala huu umeonekana kuwa mkali huku baadhi wakishindwa kukubaliana na mitazamo kwamba radio na televisheni huenda vikapoteza umaarufu siku za usoni.

Carol Wachira wanyama msimamizi wa idhara ya mauzo katika shirika la habari la Royal media nchini Kenya amesema kwamba kwa sasa aina mbili za mifumo ya usambazaji wa habari ni muhimu ijapokuwa bado mfumo wa kawaida wa radio na televisheni bado una nguvu

“Tumekuwa tukipapasa huku na huku kuweka mikakati ya kuwekeza kwenye teknolojia hii lakini ukweli ni kwamba bado hatujaweza kupata pesa tunayohitaji kutokana na mfumo wa kutangaza kupitia mfumo wa kidigitali….na wakati huo mapato kutoka matangazo ya radio na Tv yanaendelea kupungua. Kwa hiyo basi wakati tukijitahidi kuwekeza zaidi kwenye digitali hatuoni faida ya pesa tunayoitumia, lakini naamini kuwa ni suala la muda..hata hivyo ni lazima tuweke mikakati ya kuona jinsi ya kuendelea kuzalisha pesa kwa kutumia mifumo ya kawaida ya Radio na Televisheni.”

Radio, televisheni, magazeti kunufaika na mitandao ya kijamii

Craig Kelly, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Africa XP ambayo inajihusisha na kutengeneza vipindi kupitia mtandao pamoja na kusambaza mifumo ya kidigitali barani Afrika yeye amesema kwamba kuwepo kwa mitandao ya kijamii kutasaidia vyombo vya habari kubadili mifumo ya upashaji habari na kuwafikia watu wengi zaidi kuliko ilivyo sasa

‘’Nadhani swali ni kwa namna gani mifumo ya teknolojia ya kupasha habari inaweza kwenda pamoja?Na ni kwa jinsi gani watu kwenye sekta ya habari wanaelewa kuwepo kwa mahitaji haya?Pengine watu wanatakiwa kuelewa kwamba kuna namna mbalimbali…unaingia kwenye youtube unabofya unapata kile unachotaka, unaingia Netflix unabofya unaangalia kile unachotaka mara moja….wakati vyombo vya habari vya kawaida unatakiwa ukae chini utazame orodha ya vipindi unavyohitaji kuvitazama…’’

Wadau wengi katika sekta ya habari wanaamini kwamba majadiliano yanastahili kuendelea ili kupata namna ya kukabiliana na changamoto ambazo zinasababishwa na mitandao ya kijamii kwa vyombo vya habari vya kawaida.

Imetayarishwa na Sylvanus Karemera, VOA, Kigali

XS
SM
MD
LG