Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 11, 2024 Local time: 06:28

Ukraine yatupilia mbali pendekezo la Rashia la kufungua njia kwa raia wa Ukraine wanaokimbia vita


Wakimbizi wa Ukraine wakipita kwenye daraja eneo la mpaka na Poland. Machi 6, 2022. Picha ya AFP
Wakimbizi wa Ukraine wakipita kwenye daraja eneo la mpaka na Poland. Machi 6, 2022. Picha ya AFP

Ukraine Jumatatu imetupilia mbali pendekezo la Moscow la kufungua njia kwa raia wake wanaokimbia vita kutoka miji kadhaa baada ya kutambua baadhi ya njia zinaelekea Rashia na Belarus.

Naibu waziri mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk amesema “Hili pendekezo halikubaliki”, baada ya Rashia kupendekeza njia salama kwa raia kutoka miji ya Kharkiv, Kyiv, Mariupol na Sumy.

Amesema raia “hawatokwenda Belarus na baadaye wachukuwe ndege kuelekea Rashia.

Kwa upande wa mapigano, Rashia imefanya tena mashambulizi makali zaidi jana usiku kutokea angani, baharini na ardhini, na kuzidisha mzozo wa kibinadamu ambao tayari umesababisha zaidi ya watu milioni moja na nusu kuvuka mipaka ya Ukraine tangu uvamizi kuanza na kukimbilia nchi jirani.

Jeshi la Rashia limesema mapema Jumatatu kwamba limefungua njia za kibinadamu kwa ajili ya miji hiyo minne ya Ukraine.

Wachambuzi wanasema inaonekana vikwazo vya kimataifa kuiadhibu Moscow havijafanya kazi kupunguza kasi za uvamizi, na Washington imesema kwamba inajadiliana hivi sasa juu ya kupiga marufuku usafirishaji wa mafuta ya Rashia hadi nchi za Ulaya.

Bei za mafuta zilipanda Jumatatu kufikia karibu kiwango cha juu cha miaka 14 iliyopita, wakati masoko ya hisa yakishuka hii leo huku wawekezaji wakiwa na wasiwasi kutokana na athari za kiuchumi.

XS
SM
MD
LG