Kyiv ilifanya moja ya mashambulizi yake makubwa zaidi ya usiku katika wiki kadhaa, kurusha ndege zisizo na rubani zaidi ya 50 katika eneo la Russia, kulingana na wizara ya ulinzi ya nchi hiyo.
Chanzo cha usalama mjini Kyiv kililiambia shirika la habari la AFP kwamba shambulio dhidi ya kambi ya anga ya Morozovsk katika eneo la Rostov kusini mwa Russis limeharibu takriban ndege sita za nchi hiyo na nyingine nane ziliharibiwa vibaya.
Hii ni operesheni maalum muhimu ambayo itapunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa mapigano wa Warussia, chanzo kilisema, na kuongeza kuwa shambulio hilo lilitekelezwa na idara ya usalama ya SBU na jeshi.
Forum