Jeshi la Ukraine limeripoti Jumatatu limeharibu ndege mbili kati ya tatu za Russia zisizokuwa na rubani (Drone) zilizotumwa katika mashambulizi ya usiku kucha.
Ripoti hiyo haikujumuisha taarifa yoyote kuhusu wapi uvamizi huo ulifanyika, au kama kulikuwa na uharibifu wowote kutoka kwa drone ya tatu.Katika mkoa wa Belgorod nchini Russia, ambao unapakana na Ukraine, Wizara ya Ulinzi ya Russia imeripoti kuzima shambulio la Ukraine lililohusisha ndege mbili zisizokuwa na rubani.
Vyacheslav Gladkov, gavana wa mkoa wa Belgorod aliripoti uharibifu wa nyumba na umeme ikiwa ni matokeo ya vifusi viliyoanguka kutoka kwenye ndege mbili zisizo na rubani katika kijiji cha Dolgoye.
Mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak, alisema Jumatatu kwamba vita hivyo vinaendelea tu kuongeza nguvu ya Russia kwa uvamizi wake na kwamba vita kama hivyo vina suluhisho la kijeshi tu.
Forum