Idadi hii imeongezeka kutoka zaidi ya watu milioni tatu mwaka 2021.
Zaidi ya watoto laki tisa chini ya umri wa miaka mitano wana utapiamlo mkubwa. Upande wote wa kaskazini nchini humo, na sehemu kubwa ya kaskazini-mashariki, wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kufikia kiwango cha dharura, data zimeonyesha.
Kipindi cha mvua cha mwezi Machi hadi May kimekuwa chini, kisicho cha kawaida katika maeneo mengi yenye matatizo jambo ambalo limeathiri uzalishaji wa chakula.
Licha ya kuwa na ukame wa muda mrefu , mzozo umeharibiwa zaidi na kuongezeka kwa bei ya chakula kwa sababu ya kuongezeka bei ya mafuta pia, kutokana na vita vya Ukraine.
Baadhi ya nchi zilizoathiriwa zinakabiliwa na ukosefu wa usalama na vurugu zinazoendelea za ufyatuaji wa risasi.
Eneo kubwa la mashariki mwa Afrika limekabiliwa na ukame mkubwa katika mwaka huu wa 2022, hali ya ukosefu wa usalama wa chakula pia inatokana na janga la corona.