Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:52

Ukiukaji haki za binadam uliongezeka DRC 2011


Vijana wanaoaminika ni wa upinzani wakilazimishwa na polisi kuingia ndani ya gari baada ya kukamatwa mjini Kinshasa
Vijana wanaoaminika ni wa upinzani wakilazimishwa na polisi kuingia ndani ya gari baada ya kukamatwa mjini Kinshasa

Ripoti ya muungano ya mashirika yasiyo ya kiserikali huko DRC inaeleza kwamba ukiukaji wa haki za binadam uliongezeka kutokana na vitendo vya kikatila vinavyofanywa na waasi.

Ripoti iliyotolewa siku siku ya Alhamisi na muungano wa mashirika ya kiraia ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inazingatia jinsi usalama ulivyozorota hasa huko mashariki ya nchi.

Naibu mkurugenzi wa mungano huo Omar Kavota anasema miongoni mwa yale yanayothibitisha kuzorota kwa usalama na kuongezeka ukiukaji wa haki za binadam ni pamoja na visa vya mauwaji, ubakaji, unyanyasaji barabarani, na waasi ambao baado wanaendesha shughuli zao huko mashariki ya Congo.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Bw.Kavota anasema ripoti yao inatoa wito kwa serikali kupatia kipaumbele juhudi za kurudisha usalama katika jimbo la Kivu ya Kaskazini. Zaidi ya hayo anasema, wameitaka serikali kujingiza kati katika kupambana na ukiukaji wa haki za binadam na kuhakikisha vikosi vya usalama vinalipwa mishahara kwa wakati muafaka.

Bw. Kavota anasema wameitaka pia serikali kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria watu wanaokiuka haki za binadam. Na kwamba ripoti yao inalengo la kuwahamasisha viongozi wepya kufuatia uchaguzi mkuu ulofanyika mwisho wa mwaka 2011

XS
SM
MD
LG