Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 11:14

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan


Mchunguzi wa Umoja wa mataifa akisalimiana na mkuu wa Polisi.

Ujumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa umewasili katika mkoa wa Darfur

Ujumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa umewasili katika mkoa wa Darfur nchini kama sehemu ya ziara ya nchi nzima kabla ya kura ya maoni iliyopangwa kufanyika mwezi Januari.

Jeshi la Sudan linasema lilivamia maeneo ya waasi katika mkoa wa Darfur, saa kadhaa kabla ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuwasili mkoani humo. Msemaji wa kundi hilo la waasi alithibitisha shambulizi hilo,lakini alikataa kuwa waasi walifukuzwa kutoka kwenye maeneo yao.

Kabla ya kuwasili katika mkoa wa Darfur, ujumbe huo ulikutana Juba na rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, ambaye aliwahakikishia kwamba kusini haitajitenga na upande wa kaskazini ikiwa kura ya maoni itacheleweshwa.

Ujumbe huo haukukaribishwa vizuri huko Darfur,ambapo mamia ya waandamanaji wanaoiunga mkono serikali na wafuasi wa rais Omar al-Bashir, waliimba nyimbo za kumuunga mkono rais wao.

Bwana Bashir amefunguliwa mashtaka na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita -ICC huko The Hague, kwa tuhuma za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa katika eneo hilo la Sudan.

XS
SM
MD
LG