Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 16, 2025 Local time: 22:51

Ujumbe wa Marekani kuhusu uhuru wa dini umekatisha ziara yake Saudi Arabia


USCIRF
USCIRF

USCIRF imesema ujumbe ulikuwa ukitembelea Diriyah mji wa kihistoria ambao ni eneo la Urithi wa Dunia la UNESCO

Ujumbe wa Marekani kuhusu uhuru wa dini umesema Jumatatu kuwa umekatisha ziara yake nchini Saudi Arabia baada ya mmoja wa wanachama wake kutakiwa kuvua vazi lake la kichwani linalovaliwa na Wayahudi, au kippah.

Tume ya Marekani ya Kimataifa ya Uhuru wa Dini (USCIRF) imesema ujumbe wake ulikuwa karibu na Riyadh ukitembelea Diriyah, mji wa kihistoria ambao ni eneo la Urithi wa Dunia la UNESCO, wakati mwenyekiti wa tume hiyo, Rabbi Abraham Cooper, alipokataa maombi ya kumtaka avue kofia ya kidini aliyovaa kichwani.

Hakuna mtu anayepaswa kunyimwa fursa ya kuingia katika eneo la urithi, hasa mtu ambaye azma yake ni kuonyesha umoja na maendeleo, kwa kuwa ametokeza tu kama Myahudi, Cooper alisema katika taarifa.

USCIRF ilisema Cooper na makamu wake Mchungaji Frederick Davie walialikwa kutembelea eneo hilo Jumanne iliyopita kama sehemu ya ziara yao rasmi, baada ya kucheleweshwa mara kadhaa kwa ziara hiyo, maafisa waliomba Cooper avue kippah yake, wakati akiwa kwenye eneo hilo na wakati wowote alipokuwa hadharani, japokuwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia iliidhinisha ziara hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG