Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 14:34

Ujumbe wa Hamas umewasili Cairo


Ujumbe wa Hamas ukiongozwa na afisa wake mwandamizi Khalil al-Hayya, utawasili jijini Cairo, Jumamosi kuwasikiliza wapatanishi katika mazungumzo ya sasa ya kusimamisha mapigano ya Gaza ambayo yanafanyika katika mji mkuu wa Misri, kundi hilo la Palestina limesema katika taarifa.

Vyanzo viwili vya usalama vya Misri vimesema kwamba ujumbe wa Marekani, na Israel ulianza duru mpya ya mkutano Alhamisi, mjini Cairo kwamba mazungumzo ya sasa ya siku mbili yalilenga kuondoa tofauti zilizopo za shauri hilo la kusimamisha mapigano.

Hamas imeahidi nia yao kwa kile kilicho pitishwa Julai 2 ambacho kilitokana na mapendekezo ya rais wa Marekani, Joe Biden, na utayari wa kuutekeleza, amesema afisa wa Hamas, Izza al-Rishq, Jumamosi.

Forum

XS
SM
MD
LG