Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 05:02

Ujumbe wa ECOWAS watupilia mbali mkutano Mali


Maandamano ya kuunga mkono wanajeshi waasi Bamako, Mali Machi 28, 2012
Maandamano ya kuunga mkono wanajeshi waasi Bamako, Mali Machi 28, 2012

Ndege ya rais Alassane Ouattara yarudi Abidjan

Ujumbe wa marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Magharibi umetupilia mbali mpango wa kukutana na viongozi wa wanajeshi waasi kufuatia ripoti kuwa kuna maandamano ya kuunga mkono mapinduzi ya serikali kwenye uwanja wa ndege katika mji mkuu Bamako. Ujumbe huo wa ECOWAS ulijumwisha marais wa Ivory Coast, Benin, Niger na Burkina Faso na ulitegemewa kukutana Alhamis katika mji mkuu wa Mali kuomba wanajeshi hao kurejesha uatwala wa kikatiba. Mshauri wa rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara anasema ndege ya rais huyo iliingia katika anga ya mali lakini ikabadili njia na kuondoka kwa sababu kulikuwa na maandamano kwenye uwanja wa ndege. Vyanzo vya habari vya kidplomasia vinasema pia marais wa nchi hizo nyingine walifuta mpango wa kwenda kwenye mkutano huo. Viongozi wa jumuiya hiyo ya ECOWAS wanatazamiwa kufanya mkutano wa dharura mjini Abidjan.

XS
SM
MD
LG