Bai Lowe amehukumiwa kwa ukatili dhidi ya binadamu, mauaji na jaribio la mauaji, wakati alipokuwa dereva wa kundi hilo kwa jina la Junglers. Waendesha mashitaka walikuwa wameiomba mahakama kwenye mji wa kaskazini wa Celle watoe hukumu ya kifungo cha maisha kwa Lowe ambaye alikanusha mashitaka yote dhidi yake.
Kundi la Junglers lilitumiwa na Jammeh alipokuwa rais wa Gambia kuuwa watu, miongoni mwa maovu mengine, kwa lengo la kuukandamiza umma wa Gambia, na kuzima upinzani, kulingana na viongozi wa mashitaka kwenye kesi hiyo.
Miongoni mwa hatia alizopatikana nazo ni pamoja na mauaji ya mwanahabari wa AFP Deyda Hydara, ambaye alipigwa risasi akiwa kwenye gari lake kwenye kitongoji cha mji mkuu wa Gambia wa Banjul, Decemba 16, 2004. Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa mwaka jana ni ya kwanza inayoshugulikia ukiukwaji wa haki za binadamu uliotendwa nchini Gambia wakati utawala wa Jammeh.
Forum