Maafisa walisema watu 25 wamekamatwa. Waendesha wa mashtaka wa serikali wamesema baadhi ya maafisa 3,000 walifanya msako katika sehemu 130 katika majimbo 11 kati ya 16 ya Ujerumani dhidi ya wafuasi wa vuguvugu linaloitwa Reich Citizens.
Baadhi ya wanachama wa vuguvugu hilo wanakataa katiba ya Ujerumani baada ya vita na wametaka kuiangusha serikali.
Waziri wa Sheria Marco Buschmann alielezea uvamizi huo kama "operesheni ya kupambana na ugaidi," akiongeza kuwa washukiwa hao wanaweza kuwa walipanga mashambulizi ya silaha dhidi ya taasisi za serikali.
Facebook Forum