Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 07:46

Uingereza yasema Ukraine inaweza kushambulia vifaa vya Russia


Mwanamme aliyebeba baiskeli akipita karibu na gari la kijeshi la Russia lililoharibiwa
Mwanamme aliyebeba baiskeli akipita karibu na gari la kijeshi la Russia lililoharibiwa

Waziri wa ulinzni wa Uingereza Ben Wallace amesema kwamba itakuwa sahihi kwa wanajeshi wa Ukraine kushambulia vifaa vya Russia ili kuzuia usambasaji wake wa chakula, mafuta na risasi, bil akutumia silaha za Uingereza.

Hali ya mivutano imeongezeka wiki hii baada ya Moscow kuishutumu Uingereza kwa kile imekitaja kama kuichochea Ukraine kushambulia sehemu muhimu ndani ya Russia.

Russia imesema kwamba hatua hiyo itajibiwa kwa haraka sana na kwa uzito unaostahili.

Wallace amesema kwamba kulingana na sheria ya kimataifa, Ukraine ina haki ya kujilinda kwa kila namna.

Alisema kwamba kama sehemu ya kujilinda, Ukraine inaweza kushambulia sehemu ambazo Russia inaweka chakula, mafuta na risasi ili kumaliza uvamizi wa Russia.

Uingereza imekuwa ikiiunga mkono Ukraine tangu uvamizi wa Russia ulipoanza mwezi Februari, na imekuwa ikutuma misaada ya silaha kwa Ukraine kuisaidia kupambana na Russia, japo imesema kwamba haitatuma makombora ya masada marefu kwa Ukraine.

XS
SM
MD
LG