Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 13:07

Uingereza yapendekeza wanawake waislam wafundishwe kiingereza


Baadhi ya wanawake wa kiislam katika jamii ya waislam nchini Uingereza
Baadhi ya wanawake wa kiislam katika jamii ya waislam nchini Uingereza

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroon alikosoa kile anachokiita “kutostahmiliana vya kutosha ” katika jamii ya wa-Islam nchini Uingereza kwa kuwatenga na kuwabagua wanawake na alisema ufahamu mdogo wa lugha ya kiingereza unawasababisha wanawake wa ki-Islam kuwa hatarini kurubuniwa na gumzo la itikadi kali.

Makala ya bwana Cameroon iliyochapishwa Jumatatu na gazeti la The Times ilikosolewa haraka na wakosoaji ambapo alipendekeza takribani dola milioni 30 katika kugharimia madarasa ya lugha ya kiingereza kwa wanawake waislam. Pia alipendekeza baadhi ya wahamiaji wataweza kufukuzwa nchini Uingereza kwa kushindwa kuzungumza lugha ya ki-ingereza.

Sayeeda Warsi
Sayeeda Warsi

Wakati huo huo mbunge wa zamani na m-conservative, Sayeeda Warsi, mwanamke wa kwanza muislam katika baraza la mawaziri nchini Uingereza alipongeza pendekezo la kugharimia mafunzo ya lugha ya kiingereza. Lakini aliiambia radio moja ya Uingereza kwamba mapendekezo ya bwana Cameroon ni matokeo ya “uzembe na fikra potovu” dhidi ya desturi za jamii ya waislam wa nchini Uingereza.

XS
SM
MD
LG