Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 11, 2024 Local time: 06:21

Uingereza yaomba radhi na kuwalipa fidia wapiganaji wa Mau Mau Kenya


walokaa kutoka kushoto hali kulia ni wa Kenya Jane Muthoni Mara, Wambogo Nyingi and Paulo Muoka Nzili wakisherekea tangazo la kushinda kesi ya wapiganaji wa Mau Mau na kulipwa fidia.
walokaa kutoka kushoto hali kulia ni wa Kenya Jane Muthoni Mara, Wambogo Nyingi and Paulo Muoka Nzili wakisherekea tangazo la kushinda kesi ya wapiganaji wa Mau Mau na kulipwa fidia.
Serikali ya Uingereza imeomba radhi na kukubali kuwalipa fidia maelfu ya wapiganaji wa vita vya uhuru wa Kenya vilivyojulikana kama Mau Mau, kutokana na kuteswa na kutendewa maovu mnamo miaka ya 1950. Hatu hii inaweza kufungua mlango kwa mashtaka mengine dhidi ya Uingereza kwa hatua zake katika makoloni yake ya zamani.

Vita vya kupigania uhuru vilivongozwa na wazalendo wa mau Mau yalikandamizwa kikatili na serikali ya kikoloni ya Uingereza. Tume ya Haki za binadam ya Kenya inakadiria kwamba Wakenya 90,000 waliuliwa au kukatwa viungo vyao na karibu 160,000 kufungwa. Mateso na ubakaji vilikuwa vitendo vya kawaida.

Ripoti ya Mwai Gikonyo - 3:14
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:14 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Miaka 50 baadae, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza William Hague aliomba radhi siku ya Alhamisi na kukubali kulipa fidia.

"Makubaliano ni pamoja na malipo ya jumla ya dola milioni 30.8 kwa watu 5,228. Serikali itasaidia katika ujenzi wa makumbusho mjini Nairobi kwa ajili ya waathiriwa wa mateso na kutendewa maovu wakati wa enzi ya ukoloni," alisema Bw Hague.

Huko Kenya wapiganaji wa Mau Mau na waungaji mkono wao walisherehekea kwamba Uingereza imeomba radhi lakini wanasema fidia haijatosha kamwe.

Akizungumza na Sauti ya Amerika katibu mkuu wa chama cha mashujaa wa vita vya Mau Mau, Dr. Gitu wa Kahengeri alisema wameridhika kwa sehemu, lakini dola 3,500 atakayolipwa kila moja wao ni kidogo sana.

"Hivi sasa tutajaribu kuzungumza na serikali ya Kenya juu ya kutulipa fidia kwa kutupatia mashamba, lakini ikishindikana tutaifikisha serikali mahakamani."

Mahojiano na Gitu wa Kahengeri - 3:58
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:58 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Wakili aliyewawakilisha wapiganaji wa Mau mau, Martin Day anasema, hili limekua somo la kihistoria kwa Uingereza.

Uingereza ilijaribu kwa miaka mitatu kuzuia mashtaka hayo kuendelea, ikitoa hoja kwamba uwajibikaji unabidi uwe upande wa Kenya baada ya kunyakua uhuru wake 1963 na kwamba mashtaka yamefikishwa baada ya muda wa kisheria kupita, lakini hioja hizo zilipingwa na mahakama.
XS
SM
MD
LG