Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:28

Uingereza kupeleka washauri wa kijeshi Libya kuwasaidia waasi


Waasi wa LIbya wanakagua magari mawili ya wanajeshi wanaomuunga mkono Gadhafi. Waasi wanasema magari hayo yaliharibiwa na mashambulizi ya NATO.
Waasi wa LIbya wanakagua magari mawili ya wanajeshi wanaomuunga mkono Gadhafi. Waasi wanasema magari hayo yaliharibiwa na mashambulizi ya NATO.

Waasi nchini Libya watasaidiwa kufanya kazi kwa utaratibu katika kupambana na majeshi yanayomuunga mkono Moammar Gadhafi

Uingereza inapeleka washauri wa kijeshi nchini Libya kuyasaidia majeshi ya waasi yaliyozingiwa.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, William Hague amesema leo Jumanne kuwa timu yenye ujuzi ya dazeni ya washauri wa kijeshi watawasaidia waasi kufanya kazi kwa utaratibu, kiufundi na kwa mawasiliano. Hague amesema washauri hawajihusisha na mashambulizi ya kijeshi dhidi ya majeshi yanayoiunga mkono serikali ya Libya au kuwapatia silaha.

Wakati huo huo, maafisa wa NATO wamesema hivi leo kuwa kuna viwango katika kutumia nguvu ya anga kuwalinda raia wa Libya.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Alain Juppe amekiri kuwa hali ni ngumu nchini Libya, lakini amesema Ufaransa inapinga kupeleka majeshi ya ardhini kuvunja mvutano wa kijeshi.

Ndege za kivita za NATO zimepiga mabomu malengo kadhaa karibu na mji mkuu wa Libya, Tripoli hivi leo.

Ushirika umesema mashambulizi yamelenga vituo vikuu vya operesheni za kijeshi pamoja na miundo mbinu ya mawasiliano. Wizara ya ulinzi ya Uingereza imetoa picha ya mashambulizi dhidi ya mfumo wa mawasiliano wa Libya, ikisema ndege zimepiga eneo hilo mara saba katika muda wa dakika saba siku ya Jumatatu.

XS
SM
MD
LG