Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:26

Uingereza na Uswisi wanatengeneza aina mpya ya dozi mbili za chanjo ya COVID


Mkazi wa London akipata chanjo ya COVID
Mkazi wa London akipata chanjo ya COVID

Chanjo hiyo ni chanjo inayotokana na Adenovirus ambayo kulingana na klinik ya Mayo imebadilishwa na hivyo haiwezi kuunganishwa kwenye DNA ya mtu na kupelekea wawe wagonjwa

Kampuni ya kutengeneza dawa ya Uingereza na Uswisi, AstraZeneca na chuo kikuu cha Oxford wanasema wanatengeneza aina mpya ya dozi mbili za chanjo ya COVID-19 ambayo itatoa ulinzi haswa dhidi ya aina mpya ya kirusi cha Omicron katika virusi vya Corona.

Chanjo hiyo ni chanjo inayotokana na Adenovirus ambayo kulingana na klinik ya Mayo imebadilishwa na hivyo haiwezi kuunganishwa kwenye DNA ya mtu na kupelekea wawe wagonjwa. Chanjo ya Johnson and Johnson inayotolewa kwa dozi moja pia inategemea Adenovirus.

Sandy Douglas kiongozi wa kikundi cha utafiti huko Oxford aliliambia gazeti la Financial Times kwamba chanjo zenye msingi wa Adenovirus zinaweza kutumika kujibu aina yeyote mpya ya virusi kwa haraka zaidi kuliko ambavyo wengine wangegundua hapo awali.

XS
SM
MD
LG