Wanasayansi wanasema kwamba kirusi cha BA.2.86, ambacho ni kutokana na kile cha Omicron huenda kisisababishe maradhi au vifo kutokana na kinga iliyoletwa na chanjo za awali kote ulimwenguni. Hata hivyo wizara ya afya ya Uingereza imesema kwamba program ya chanjo ya kila mwaka kwa wakongwe pamoja na makundi yaliopo hatarini itaanza wiki kadhaa kabla ya muda wake kutokana na kirusi hicho kipya.
Kirusi hicho kiligundulika mara ya kwanza Uingereza hapo Agosti 18, wakati zoezi la chanjo likipangwa kuanza Septemba 11, miongoni mwa wakazi waliyopo kwenye nyumba za wazee, pamoja wa wale waliyopo kwenye hatari zaidi ya maambukizi. Wizara hiyo imeongeza kusema kwamba bado kirusi hicho hakijaorodheshwa kuwa hatari nchini humo, na kwa hivyo hakuna haja ya kuweka kanuni mpya za kuzuia maambukizi kwa umma.
Forum