Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:15

Uingereza imetoa taarifa ya kijasusi kuhusu Russia


Rais wa Russia, Vladimir Putin
Rais wa Russia, Vladimir Putin

Wizara ya ulinzi ya Uingereza ilisema utoaji huo wa taarifa "ni utaratibu muhimu wa kuendeleza matumizi ya ulinzi, ambayo yameongezeka kwa kiasi kikubwa tangu uvamizi wa Ukraine". Russia imetangaza bajeti ya ulinzi ya 2023 ya takribani dola bilioni 84

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema katika taarifa yake ya kijasusi Jumamosi kwamba Russia ilifanya "utoaji wake mkubwa zaidi wa madeni katika siku moja".

Utoaji huo, wizara hiyo ilisema, "ni utaratibu muhimu wa kuendeleza matumizi ya ulinzi, ambayo yameongezeka kwa kiasi kikubwa tangu uvamizi wa Ukraine."

Utoaji huo ulikusanya dola bilioni 13.6, kulingana na taarifa mpya iliyochapishwa kwenye Twitter.

Russia imetangaza bajeti ya ulinzi ya 2023 ya takriban dola bilioni 84, ikiwa juu kwa asilimia 40 kuliko bajeti yake ya awali ya 2023 iliyotangazwa mwaka 2021.

"Ukubwa wa mnada huu," Wizara ya Ulinzi ilisema, "kuna uwezekano mkubwa inaonyesha Wizara ya Fedha ya Russia inaona hali ya sasa kama nzuri lakini inatarajia mazingira ya kifedha yanayozidi kutokuwa na uhakika katika mwaka ujao."

Katika mahojiano na shirika la habari la Associated Press, meya wa jiji hilo, Vitali Klitschko, alisema mamlaka zinajaribu kurejesha umeme katika jiji hilo.

Mashambulizi ya anga ya Russia yamesababisha uharibifu mkubwa kwenye gridi ya nishati ya mji mkuu wa Ukraine huku yakiendelea kuishambulia Ukraine katika maeneo mengi ya nchi - kutoka Kyiv kaskazini hadi Odesa kusini na kusambaratisha karibu nusu ya mfumo wa nishati wa Ukraine, Waziri Mkuu wa Ukraine Denys Shmyhal alisema.

XS
SM
MD
LG