Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:51

India yakanusha ripoti kuhusu ukandamizaji wa uhuru wa dini


Muandamanaji aliyejifunika uso akikimbia mawe yanayorushwa na polisi wa India kwenye maandamano ya Srinagar katika Kashmir inayodhibitiwa na India.
Muandamanaji aliyejifunika uso akikimbia mawe yanayorushwa na polisi wa India kwenye maandamano ya Srinagar katika Kashmir inayodhibitiwa na India.

India imekanusha vikali madai yaliyotolewa na tume moja ya Marekani kwamba uhuru wa dini upo kwenye mtazamo mbaya nchini humo.

Tume ya kimataifa ya uhuru wa dini Marekani (USCIRF) hivi karibuni ilitoa ripoti iliyosema ustahmilivu wa kidini umepungua na ghasia za uhuru wa dini ziliongezeka nchini India katika mwaka 2015.

Wizara ya mambo ya nje ya India ilisema haitakubaliana na ripoti hiyo ambapo ilisema imeshindwa kuonyesha uwelevu sahihi wa India, jamii yake na katiba yake.

Ripoti ya USCIRF ilisema jamii za walio wachache nchini India hususan wakristo, waislamu na singa singa wameshuhudia matukio mbali mbali ya manyanyaso na ghasia kwa kiasi kikubwa kwenye mikono ya makundi ya wahindu.

XS
SM
MD
LG