Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 03, 2023 Local time: 04:37

Rais Kenyatta akutana na Raila Odinga


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, siku ya Jumanne alikutana na kiongozi wa muungano wa Kisiasa wa CORD, Raila Odinga, katika Ikulu ya Nairobi.
Wawili hao walikutana alasiri wakati wa chakula cha mchana kwa heshima ya rais Park Guen-Hye wa Korea Kusini ambaye yuko ziarani nchini Kenya.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, siku ya Jumanne alikutana na kiongozi wa muungano wa Kisiasa wa CORD, Raila Odinga, katika Ikulu ya Nairobi. Wawili hao walikutana alasiri wakati wa chakula cha mchana kwa heshima ya rais Park Guen-Hye wa Korea Kusini ambaye yuko ziarani nchini Kenya.

Na BMJ Muriithi

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, siku ya Jumanne alikutana na kiongozi wa muungano wa Kisiasa wa CORD, Raila Odinga, katika Ikulu ya Nairobi.

Wawili hao walikutana alasiri wakati wa chakula cha mchana kwa heshima ya rais Park Guen-Hye wa Korea Kusini ambaye yuko ziarani nchini Kenya.

Taarifa kutoka kwa msemaji wa Ikulu imesema kuwa baadaye, Kenyatta na Odinga walifanya mkutano uliohudhuriwa pia na naibu wa Rais William Ruto na kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetang'ula.

Kabla ya mkutano huo, Bwana Odinga alikatiza ziara yake katika kaunti ya Narok ambako alitarajiwa kuhudhuria mazishi, na badala yake akawaambia waombolezaji kiwamba rais Kenyatta alikuwa amempigia simu kutaka wakutane mjini Nairobi.

"Nimepata simu kutoka kwa State House niende nizungumze na Uhuru Kenyatta. Naomba ruhusa yenu kama watu wa Narok niende nizungumze na yeye tukielewana nitawaambia Wakenya, tusipozungumza pia nitawajulisheni," akasema Raila.

Kiongozi huyo wa chama cha ODM alikuwa ameenda kuhudhuria mazishi ya mke wa mwanachama wa kwanza wa seneti baada ya Uhuru Bw Lemein katika kijiji cha Motonyi, kaunti ndogo ya Narok Kaskazini.

Haya yamejiri huku hali ya wasiwasi ikitanda baada ya kiongozi huyo wa upinzani kutangaza kwamba atakaidi amri na kufanya mkutano sambamba na ule wa maadhimisho ya sikukuu ya Madaraka, siku ya Jumatano.

Upinzani umekuwa ukiitisha mkutano wa kujadili maswala ambayo unasema ungependa yashughulikiwa kabla ya uchaguzi wa mwaka ujao.

Raila meets with Kenyatta
Raila meets with Kenyatta

Awali, serikali ilitangaza kwamba hakuna mikutano ingefanyika sambamba na ule wa Madaraka, ambao unatarajiwa siku ya Jumatano kwenye uwanja wa Afraha, mjini Nakuru.

Jumanne alasiri, gazeti la Daily Nation liliripoti kwamba Odinga na Kenyatta walikuwa wanaendelea na mkutano wao katika Ikulu.

Picha zilizotolewa na Ikulu ya Nairobi zilimuonyesha Odinga akila chakula cha mchana katika Ikulu na akiketi katikati ya mbunge wa Jubilee Adan Duale na Waziri wa usalama wa ndani, Joseph Nkaisery, ambao wamekuwa wakosoaji wake kwa misimamo yake ya kisiasa.

Kiongozi huyo wa ODM alinukuliwa akisema kwamba ana furaha kwa sababu rais Kenyatta alimpigia simu akitaka mazungumzo na kwamba alitumaini kuwa makubaliano kuhusu maswala nyeti - pamoja na lile la kutaka kuondolewa kwa maafisa wa tume ya uchaguzi kabla ya uchguzi mkuu wa mwaka kesho - yataafikiwa.

XS
SM
MD
LG