Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:38

Uhuru akosolewa kwa kutounda jopo la jaji Tunoi


Rais Uhuru Kenyatta amesema kwamba hataunda jopo kazi la kumchunguza jaji wa mahakama kuu nchini humo, Philip Tunoi, ambaye anakabiliwa na shutuma za kupokea rushwa ya kiasi cha shilingi milioni mia mbili ili kuamua kesi kwa njia ya kumpendelea mshtakiwa.
Rais Uhuru Kenyatta amesema kwamba hataunda jopo kazi la kumchunguza jaji wa mahakama kuu nchini humo, Philip Tunoi, ambaye anakabiliwa na shutuma za kupokea rushwa ya kiasi cha shilingi milioni mia mbili ili kuamua kesi kwa njia ya kumpendelea mshtakiwa.

Kiongozi wa chama United Democratic Party, Cyrus Jirongo, amemkosoa rais Uhuru Kenyatta kawa kukataa kuunda jopo kazi la kumchunguza jaji wa mahakama kuu nchini humo, Philip Tunoi, ambaye anakabiliwa na shutuma za kupokea rushwa ya kiasi cha shilingi milioni mia mbili ili kuamua kesi kwa njia ya kumpendelea mshtakiwa.

Siku ya Jumatatu rais Kenyatta alisema kuunda jopo hilo kungezua mzozo wa kikatiba kwa sababu tayari mahakama ya juu ilikuwa imeamuru kwamba Tunoi alifaa kustaafu lakini jaji huyo akakata rufaa. Kenyatta alisema hawezi kuchukua hatua yoyote hadi kesi kuhusu iwapo Tunoi amefikisha umri wa kustaafu au la isikizwa na kuamriwa na mahakama ya rufaa

Lakini Jirongo ambaye alizungumza na Sauti ya Amerika siku ya Jumatatu - muda mfupi baada ya rais Kenyatta kukutoa kauli hiyo - alisema si haki kwa Kenyatta kukataa kuunda tume ya kumchunguza jaji huyo kwa sababu katiba inamtaka afanye hivyo. Haya hapa mahojiano ya BMJ Muriithi na mbunge huyo wa zamani:

please wait

No media source currently available

0:00 0:05:20 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG